Kuuliza kwangu ni kitu cha kawaida endapo sijafahamu ninachoelekezwa au kufundishwa na hapo nitarudia kuuliza kwa msisitizo kwamba maelekezo niliyoyapata yalikuwa sahihi?wengi wetu uona kwamba kuuliza ni moja ya kujiona ni mjinga kitu ambacho si sahihi.unapouliza uenda hujaelewa ili ueleweshwe vyema au umeelewa na unauliza ili kumuhakikishia yule aliyekuelekeza au kukufundisha kwamba umeelewaje.Pendelea kuuliza kwani kuuliza sio ujinga na ukipendelea kuuliza uliza hii itakusaidia kujifunza mengi sana.
Furaha ya watoto wewe unaichukuliaje? binafsi nikiona watoto wanafuraha huichukulia furaha ile kama ni Amani kwa upande wangu,kwani mtoto anapoumwa ndani ya nyumba basi watu wote hukosa amani na kuona nyumba imepooza.Napenda sana watoto na napenda sana haki za watoto,tuwapende watoto zetu na kuwapa haki stahiki kila inapobidi,tujifunze tulikotoka,tuangalie nini tulikosa na kwanini? nini tunapaswa kuwafanyia watoto wetu ili kuwapa matumaini ya makuzi yao.Furaha kwa mtoto ni amani kwenye nyumba na makuzi bora kwa mtoto ni moja ya akili na maarifa bora toka kwa wazazi na hii itakusaidia jinsi ya kuwafundisha watoto na kujua majukumu yako na yao kwa maisha ya baadae.
Nikitulia sehemu nzuri yenye mchanganyiko wa majani na maua huwa najifunza mengi sana kutokana na mahala hapo.
kwanza napenda sehemu tulivu ili kutuliza akili yangu,pili napenda ile hali ya mchanganyiko wa rangi na kuifanya akili yangu na nafsi yangu kuwa na burudani ndani ya moyo wangu.
Napenda sehemu safi na tulivu na napenda kujifunza mengi kutokana na hali hiyo.
Na ndio maana hupendelea kila siku au kila mara kuchagua sehemu tofautitofauti ili kuiweka akili yangu katika hali ya upya fulani,Akili ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku ya mwanadamu na unapokuwa na akili nzuri itakusaidia kufanya mambo yako kwa vile jinsi unavyopenda kufanya,na unapokuwa na akili na wanadamu wenzako watapenda kuitumia akili yako katika mambo yao.Jitahidi kujipumzisha vya kutosha ili kuipa nguvu akili yako.
Nilipokuwa mdogo nakumbuka nilikuwa nilipelekwa na wazazi wangu sehemu mbalimbali za makumbusho,nilibahatika kwenda sehemu za makumbusho ya kale kule Bagamoyo kuona majumba yaliyotumika kusafirishia watumwa,Nilipelekwa pale Makumbusho ya taifa Kijitonyama kuona nyumba za makabila mbalimbali nchini Tanzania.
Nilikwenda Kisiwani Zanzibar kuona wale kobe walioishi miaka mingi sana,nakumbuka baadhi ya vitu ambavyo niliviona na havikunitoka akilini mpaka leo,navyo ni kama visima vya maji ya kale,makaburi ya watu wa zamani pale Bagamoyo.
Pale Bagamoyo kulikuwa na mzee mmoja sijui kama bado yupo alijulikana kwa jina la Samahani Kajeli,alikuwa ni mtu mwenye kutoa historia nzuri sana ya mambo ya kale pale Bagamoyo.Tulimpenda sana kwa jinsi alivyokuwa akituelezea mambo yaliyokuwa yakifanyika siku za miaka ya nyuma pale Bagamoyo,ingawa nilikuwa mdogo ila baadhi ya mambo bado nayakumbuka.
Kutoka na kuzoeshwa na wazazi wangu kutembelea baadhi ya majumba ya makumbusho mpaka leo hii nimekuwa napenda sana kutembelea sehemu hizo kama ninavyoonekana pichani hapo juu nikiwa nje ya jumba la makumbusho jijini Brussel nchini Belgium.Napenda sana kujifunza ili nijue na hii hunisaidia sana kiakili.
Napenda kujifunza kutona na watu,nyakati na wakati na hii inanipa uzoefu kila kukicha.
Changamoto za kujifunza ni lazima uwe msikivu,mvumilivu na jasiri,usipende kukata tamaa mapema kutokana na kukatishwa tamaa na watu,nyakati au wakati.
kwani kuna kipindi hufikia watu hupendelea kukatisha tamaa wenzao,kuna kipindi nyakati huwa zinakatisha tamaa,na kuna kipindi wakati huwa pia unakatisha tamaa hivyo hupaswi kukata tamaa.
Hivyo hupaswi kukatishwa tamaa kutoka na hayo mambo matatu niliyoyataja hapo juu.Jitahidi kuipokea hali hiyo kama ni moja ya changamoto katika maisha.
Napenda kujifunza,ninaposema napenda kujifunza ni kweli napenda kujifunza na hili liwe funzo kwako.
Ahsanteni sana.
Maganga One.
1 Comments