Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akiingia katika ukumbi wa Hyatt Regency uliopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa mapango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana kiafya , kielimu na kijamii. 
Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akizindua mpango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana kiafya , kielimu na kijamii katika ukumbi wa Hyatt Regency uliopo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Husein Mwinyi akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa mapango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana kiafya , kielimu na kijamii katika ukumbi wa Hyatt Regency uliopo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daud Nasibu akitoa utambulisho wakati wa uzinduzi wa mpango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana kiafya , kielimu na kijamii katika ukumbi wa Hyatt Regency uliopo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa UN Mama Asha Rose Migiro akiongea na wadau mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana kiafya , kielimu na kijamii katika ukumbi wa Hyatt Regency uliopo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kushoto) akiongea na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa UN Mama Asha Rose Migiro wakati wa uzinduzi wa mpango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana kiafya , kielimu na kijamii katika ukumbi wa Hyatt Regency uliopo jijini Dar es Salaam. 
Viongozi mbalimbali wakkicheza wimbo wa wanawake na maendeleo ulioimbwa na msanii Vicky Kamata wakati wa uzinduzi wa mpango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana kiafya , kielimu na kijamii katika ukumbi wa Hyatt Regency uliopo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akiwa na baadhi ya wake wa viongozi mbalimbali wakifurahia uzinduzi wa Mpango wa Kasi ya Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana leo Agosti 24, 2012 katika ukumbi wa Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Wake wa viongozi wakicheza wimbo wa wanawake na maendeleo ulioimbwa na msanii Vicky Kamata wakati wa uzinduzi wa mpango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana kiafya , kielimu na kijamii katika ukumbi wa Hyatt Regency uliopo jijini Dar es Salaam.
Wake wa viongozi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kwa uzinduzi wa mpango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana kiafya , kielimu na kijamii katika ukumbi wa Hyatt Regency uliopo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akiwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt Asha-Rose Migiro baada ya Mama Kikwete kuzindua Mpango wa Kasi ya Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana leo Agosti 24, 2012 katika ukumbi wa Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam.(Picha na Anna Itenda – Maelezo).

Emmanuel Mohamed – Maelezo
Kubeba ujauzito katika umri mdogo, kutokuwa na uzazi wa mpango wa uzazi pamoja na magonjwa yatokanayo na uzazi ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha kupunguza vifo vya akina mama hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mpango kasi wa uwezeshaji wanawake na wasichana.
Amesema kuwa wasichana walio beba ujauzito katika umri mdogo wanaweza kupata matatizo mara mbili hadi mara tano zaidi na kusababisha vifo.
Mama Salma amefafanua kuwa malengo ya mpango huo ni kuboresha maeneo ya elimu kwa wasichana, usawa wa kijinsia na uzazi wa mpango kwa lengo la kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 1999 na mwaka 2010 vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano vimepungua kutoka 147 hadi 81 kwa kila vizazi hai 1,000;
Hata hivyo vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi vimepungua kutoka 578 kwa kila vizazi hai laki mmoja hadi kufikia 454.
Tawimu hizo zimetolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Mama Salma kuzindua mpango huo.
Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ina mkakati wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi na vya watoto.
DKt. Mwinyi ameongezea kuwa mpango mkakati wa Afya ya Uzazi kwa vijana umelenga kutoa huduma ya elimu na taarifa kuhusu afya uzazi ambao unalenga kupunguza kupata ujauzito katika umri mdogo.
Wakati huohuo Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Angelah Kariuki ametoa rai kwa wanawake kujitokeza kutoa maoni ya katiba kuhusu utungaji wa sheria ya kuzuia unyanyasaji wa kijinsia.