Raia 37 wa Uchina wamerejeshwa nyumbani kutoka Angola, ambako walikamatwa kwa
tuhuma za kufanya uhalifu dhidi ya Wachina wenzao.
Uhalifu huo ni pamoja na utekaji nyara, kunyang'anya watu pesa, wizi kwa
kutumia silaha, na kulazimisha wanawake wauze miili yao.
Kikosi maalumu cha polisi wa Uchina kilitumwa Angola kushirikiana na polisi
wa huko dhidi ya magengi ya Wachina yaliomo Angola.
Wizara ya Uchina ya usalama inasema magengi 12 yalivunjwa.
Wizara hiyo ilisema hii ni mara ya kwanza kwa polisi wa Uchina kufanya msako
mkubwa kama huo dhidi ya wahalifu wa Kichina katika bara la Afrika.
0 Comments