Masai mmoja alipanda matatu(daladala) na baada ya kukaa muda kidogo akagundua kuwa ameibiwa simu yake,mambo yakawa hivi;
                         
                         MAASAI:"Aliyeiba simu yangu arudishe kabila sijafanya kama Loitoktok nilipoimbiwa simu yangu ya tochi.(huku akiweka kisu chake vizuri)
                         
               Konda akaona mambo yataharibika simu isipotoka, akaamua kutangaza.
                         
                         KONDA:"Mabrazameni, aliyechukua simu ya maasai amrejeshee fasta  hatutaki kuona damu ikimwagika hapa!"
                         
                         Jamaa aliyemuibia akamrejeshea masai simu yake kwa uwoga na aibu juu. Baada ya muda konda akauliza masai
                         
                         KONDA:"Ulipoimbiwa simu yako ya tochi  Loitoktok ulifanyaje?"
                         
                         MASAI:"Unachesea mimi, niliusa ng'ombe 2 nikanunua simu ya yenye picha.....hasingerudisha leo ningeusa ng'ombe 7 ninunue blackberry!"
                         Kijana akajilaumu na kujutia kupoteza "fursa" iliyojitokeza.

                                         Jumanne njema kila mmoja.