Mshiriki wa michuano ya Olimpiki kutoka Tanzania, Zakia Mrisho, leo ameshindwa kufurukuta baada ya kuambulia nafasi ya 31 kati ya washiriki 34 waliokimbia mbio za mita 5000 kwa wanawake. Zakia amekimbia umbali huo kwa dakika 15 na sekunde 39.