Sura ya mtoto imefichwa kutokana na maadili
Huyu ni mtoto Jina Limehifadhiwa mwenye umri wa
miaka 8, alikuwa nyumbani wakati wazazi wake wote wakiwa hawapo,
Alikuwa
yeye na kaka yake mwenye umri wa miaka 12.Ndipo swahibu lilipomkuta
mpaka kufanya aumizwe kiasi hiki
Huyu ndio
mtuhumiwa baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye
hasira
|
Mtuhumiwa akipandishwa kwenye gari la
polisi
---
Alifika nyumbani na kumlaghai mtoto Jina Limehifadhiwa
kwa pipi na kumuita uncle, uncle.
Akamvuta mpaka vichakani.
Akiwa
tayari ameshashusha nguo, akataka kumlawiti.Mtoto alipoona hivyo akaanza kupiga
kelele na kupambana na mtuhumiwa.
Mtuhumiwa wa uasi alipoona mtoto
anapiga kelele, akaanza kumshambuliwa kwa kumng'ata kwa meno mashavuni na
kisha kumpiga na jiwe kwenye paji la uso.
Kwa bahati nzuri, mama
aliyekuwa anashusha matofali jirani alisikia purukushani za kelele hizo
kabla ya tendo baya la ulawiti kufanyika. Ndipo mama yule akawaita watu
ambao walimkuta mtuhumiwa akiwa anaendelea na jaribio lake hilo la
kulawiti.
Mtuhumiwa alifanikiwa kumwaga haja zake, ila hakufanikiwa
kumuingilia mtoto kimwili, ndipo watu wenye hasira walipompa adhabu yake na
yeye, kabla Polisi kufika na kumtia mbaroni.
Inasemekana kuwa
mtuhumiwa huyu ndiyo tabia yake, mitaa ya Mbezi ya Kimara, amezunguka sana
kuharibu watoto wa watu, ila hii ndio ilikuwa arobaini yake. Kila Nyumba
akifika anauliza baba na mama wapo? akijibiwaa hawap,o anaanza shughuli
zake.
Hivi sasa yuko mahututi katika Hospitali ya TUMBI, akingojea
kusomewa mashtaka.
|
0 Comments