Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma, Antony Mavunde akirejesha fomu za kugombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kwa Mkuu wa Idara ya Siasa Oganizesheni ya UVCCM Taifa, Sophia Duma. Zoezi la urejeshaji fomu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za UVCCM ulitaraji kufikia tamati jana jioni kwa wagombea wote kutakiwa kutejesha fomu zao.
Mdau Innocent Meleck nae ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti UVCCM waliorejesha fomu za kugombea nafasi hiyo leo kwa Mkuu wa Idara ya Siasa Oganizesheni ya UVCCM Taifa, Sophia Duma.
Daniel Zenda akirejesha fomu za kugombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kwa Mkuu wa Idara ya Siasa Oganizesheni ya UVCCM Taifa, Sophia Duma. 
Lulu Abas Mtemvu nae alirejesha fomu zake za kuwania Ujumbe wa NEC kupitia UVCCM.