FFU wa Ngoma Africa band wamaliza kazi Afrika-Messe,Bremen,Ujerumani

Washabiki na wapenzi wamejirusha na gwaride bila ya kuchoka,

Si ingine bali ni Ngoma Africa band aka FFU,bendi ya muziki wa dansi
yenye makao yake kule Ujerumani.
Katika maonyesho ya kibiashara ya Afrika-Messe Trade fair kule mjini
Bremen,Ujerumani,bendi hiyo maarufu kwa kupelekana puta na washabiki
wake ilikutana na washabiki au wapenzi wa muziki walio gado katika
kuyarudi mangoma siku ya jumamosi 15.9.2012 mjini Bremen.
Ambako maonyesho hayo aliudhuriwa na maelfu ya watu,Ngoma Africa band
ndio walikuwa wakisubiriwa kwa hamu,walipanda jukwaani saa 11 alasiri
na kuanza kupeleka mashambulizi ya muziki kwa washabiki ambao waliupokea
mdundo kwa kila hali.
Wasikilize FFU katika kambi yao at www.ngoma-africa.com
wasiliana nao at contact@ngoma-africa.com