Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea,Arbogast Kiwale akiwa pamoja na Balozi wa Japan Nchini Tanzania ,Masaki Okada wakitia saini mkataba wa kusaidia Ujenzi wa Mabweni mawili ya shule ya sekondari ya kutwa ya wasichana Nachingwea wenye thamani ya dola za marekani 243,698. Mkataba huo umesainiwa leo mbele ya Wabunge wa mkoa wa Lindi,Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri huku Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Katibu Tawala mkoa akishuhudia.
Wabunge wa Mkoa wa Lindi nao wakishuhudia kuwekwa kwa saini mikataba ya Kusaidia ujenzi wa Mabweni 2 ya shule ya
sekondari ya Nkowe wilayani Ruangwa Pamoja na Mabweni mawili ya Shule ya kutwa ya wasichana Nachingwea.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkowe wilayani Ruangwa Mwl Shannel Nchimbi akikabidhi hati ya makubaliano ya msaada wa mabweni 2 kwa shule hiyo kwa Balozi wa Japan, Masaki Okada hii leo katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Serikali ya Japan imetoa Jumla ya dola za kimarekani 243,698 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni 4 kwa shule za sekondari za Nkowe wilayani Ruangwa Na Shule ya kutwa ya Wasichana wilayani Nachingwea Hatua hiyo imekuja katika jitihada za Nchi ya Japan kukuza Ushirikiano na Tanzania Balozi wa Japan Nchini Masaki Okada leo amelala wilayani Ruangwa Mkoani Lindi ambapo kesho atatembelea shule ya sekondari NKOWE na Baadae kuelekea Wilayani Nachingwea