Waziri Mkuu wa zamani wa Utaliana, Silvio Berlusconi, anasema anaona anawajibika kubaki kwenye siasa ingawa amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kuhepa kodi ya mapato.Bwana Berlusconi alisema amekutikana na makosa kwa misingi ya kile alichosema ni ndoto; na kwamba inambidi aendelee na siasa apate kubadilisha mfumo wa mahakama ili kuhakikisha kuwa yaliyomkuta yeye, hayatatokea kwa wengine.
Waandishi wa habari wanasema tangazo hilo limeshangaza kwa sababu mapema juma hili Bwana Berlesconi alisema hataongoza chama chake kwenye uchaguzi wa mwakani.
Wakili wa Bwana Berlusoni anasema atakata rufaa.