Kamanda mwanadamizi wa Somalia ameuwawa alipoviziwa na kushambuliwa na kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabaab.Gavana wa jimbo la Shabelle Kusini, kusini mwa Somalia, alisema Jenerali Ibrahim Mohamed Farah Gordon na wanajeshi wengine watatu waliuwawa karibu na mji wenye bandari, mji wa Merca.
Al Shabaab - ambao wanadhibiti eneo karibu lote la kusini na kati mwa Somalia - hivi karibuni waliondoka katika miji yote mikubwa, pamoja na Merca.
Kundi hilo bado linafanya mashambulio ya kuvizia na mengineyo