Wasiwasi umetanda kisiwani Zanzibar kufuatia kutoweka kwa
kiongozi wa kidini Sheikh Farid Hadi Ahmed.
Watu wawili wametiwa nguvuni waliohusika na maandamano na ghasia
zilizosababisha uharibifu mkubwa kisiwani humo.
Kuna hofu kuwa kiongozi huyo huenda amekamatwa na polisi na anazuiliwa
Tanzania bara kutokana na kuwa amepinga utawala wa chama tawala cha Tanzania
bara CCM.
Kwingineko, hapo jana polisi nchini Tanzania walimkamata mhubiri mwenye utata
anayetuhumiwa kwa kuchochea vurugu wiki jana , na kusababisha maandamano
mapya.
Kulingana mkuu wa polisi, Suleiman Kova ,Sheikh Ponda Issa Ponda, mkuu wa
Jumuiya ya waislamu, vuguvugu ambalo halitambuliki na serikali ya Tanzania,
alikamatwa kwa kuchochea vurugu.
Kukamatwa kwa Sheikh Ponda, mini Dar es Salaam, inakuja baada ya kukamatwa
kwa watu 31 waliozua vurugu na kupora mali ya watu wakati waandamanaji walijawa
na ghadhabu na kuandamana wiki jana wakiharibu makanisa kadhaa mjini humo.
Maandamano ya wiki jana yalisababishwa na tetesi kuwa kijana mwenye umri wa
miaka kumi na miwili aliikojolea Quran.
Ponda amekuwa akiwaongoza wafuasi wake kufanya maandamano kinyume na sheria
na kutoa wito wa ghasia na umwagikaji damu mjini Dar es Salaam na nchini
kote. |
0 Comments