Wataalamu wanahofia kimbunga hicho huenda kikawa kikali mno wakati
kitakapopiga sehemu za nchi hiyo.
Baadhi ya mikutano ya kisiasa ya hadhara imesitishwa huku Rais Obama akionya
watu kuchukua hatua za kujikinga na athari za zaidi za kimbunga hicho.
Usafiri wa kimataifa kutoka nchini humo umeathirika sana. Mashirika ya ndege
ya Ufaransa, Uingereza na Virgin Atlantic yamesitisha safari zao katika baadhi
ya sehemu za nchi hiyo ikiwemo miji ya , New York, Baltimore, Newark,
Washington, Boston na Philadelphia kuanzia leo.
Kwa mujibu wa idara ya utabiri wa vimbunga, saa nane asubuhi ya leo, kimbunga
hicho, kilianza kuelekea Kaskazini kikienda kwa kasi ya kilomita 760, Kusini
Mashariki mwa mji wa New York.
Hali ya tahadhari imetangazwa katika miji ya Maryland, New York,
Pennsylvania, Virginia, Washington DC na North Carolina.
Kimbunga hiki kinatoa fursa kwa Rais Obama kuonyesha uongozi wake mbali na
siasa na ikiwa atakosa kuonyesha uongozi unaostahili huenda wakosoaji wake
wakatumia fursa hiyo kumponda na kumlaumu kwa kosa lolote. |
0 Comments