Polisi waliwahi kunasa mabomu na maguruneti ambayo Al Shabaab
walikuwa wananuia kutumia kwa mashambulizi Kenya
Takriban polisi kumi wa Kenya wamejeruhiwa vibaya katika
shambulizi la guruneti
Maafisa hao wa polisi walikuwa wanasaka nyumba moja mjini Mombasa, pwani mwa
Kenya ambako walipata silaha ikiwemo bunduki aina ya AK-47 na maguruneti mawili.
Msemaji wa polisi alidokeza kuwa wanamgambo wa Al-Shabab huenda walihusika na
shambulizi hilo.
Kenya kwa muda sasa imakumbwa na misururu ya mashambulizi ya maguruneti,
tangu wanajeshi wake walipoingia Somalia kupambana na wanamgambo wa Al Shabaab
mwaka jana.
Mkuu wa Polisi mkoani humo, Aggrey Adoli,aliambia waandishi wa habari kuwa
washukiwa watatu wa kigaidi waliuawa katika makabaliano kati yao na polisi baada
ya shambulizi hilo.
Washukiwa wa Al-Shabab wametekeleza mashambulizi kadhaa katika kipindi cha
mwaka mmoja uliopita eneo la Pwani ambalo ni maarufu kwa watalii.
Wanajeshi wa Kenya nao wamekuwa vitani kuondoa kundi la Al Shabaab kutoka
katika ngome yao kubwa na ya mwisho ambayo ni Kismayo kwa ushirikiano na
wanajeshi wa Muungano wa Afrika tangu Oktoba mwaka jana, jambo ambalo
walifanikisha mwanzoni mwa mwezi huu. |
0 Comments