| Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akijaribu kumtoka beki wa Kagera Sugar wakati wa mchezo wao uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.TIMU ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam imelazimishwa sare ya bao 2-2 na Kagera Sugar ya mjini Bukoba kwenye mchezo uliopigwa jana ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Wekundu hao yamewekwa kimiani na Felix Sunzu pamoja na Mrisho Ngassa wakati ya Kagera Sugar yakifungwa na Themi Felix pamoja na beki wa zamani wa Simba, Salum Kanoni aliyefunga kwa penati. |
0 Comments