Katika sherehe yetu ya Eid El Hajj hapo jana tulibahatika kutembelewa na Ustadh Mkubwa toka Brussel nchini Belgium,Ustadh Ahmad ambaye alitupa mawili matatu na kutuombea Duaa,Mungu amjaalie kwa kila jema alilotupa hapo jana kwenye siku nzuri.

Bidada Azza akitoa maelekezo kwa mzungu kuhusu vyakula vya kiafrika vilivyo na test na ni fresh,kila mtu alijiramba kwa utamu wa vyakula mezani
Wageni wetu waalikwa wakipata picha muda mfupi tu baada ya kuwasili kwenye sherehe za jana
Bidada Fatma a.ka. Fatma Mashauzi Classic akiwa na mwanawe Maysaira na bidada Muu walipata kumbukumbu ya pamoja hapo jana.
Mama Fatma kulia akifurahia vyema Eid hapo jana,kulia kwake ni dada yake toka Uingereza nae alikuja kutupa sapoti kwenye shughuli nzima ya hapo jana.Shukrani zake za dhati na Allah atamlipa insh`Allah.
Toka nchini France ni mama na mwana,tunashukuru kwa kweli kwa wageni toka kila kona ya Ulaya kwa kuja kujumuika nasi...Allah atawalipa kwa wema wenu insh`Allah.
Toka nchini Holland napo tulipata wageni wengi sana...tunawashukuru sana kwa ukarimu na wema wenu.
Hawa ni wa hapa hapa.....wageni wetu ambao wao wapo ndani ya Ubelgiji nao hawakututupa mkono.
OOoooopssss..!!! mimi,mke wangu na shemeji yangu mama Kareem kwa nyuma tukipata kumbukumbu ya Eid El Hajj hapo jana.
Kwenye wakubwa ujue na wadogo wapo na kwenye wazee kubali kwamba kuna Vijana...pichani ni vijana ambao nao walijumuika nasi katika sikukuu nzima ya Eid.     ILI UONE  PICHA ZAIDI SHUKA CHINI YA HII PAGE.