Mahakama ya jinai ya kimataifa mjini Hague, ICC, imekataa rufaa ya rais wa
zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, kwamba aachiliwe kwa dhamana kabla ya
kesi yake kuanza.Jaji kwenye kesi hiyo, Sanji Monagan, alisema mahakama imetenda haki:
"Mahakama ya rufaa inaona kuwa katika hali hii, uamuzi wowote katika mahakama
ya kabla ya kesi, kuhusu Bwana Gbagbo kuendelea na kifungo au kuachiliwa kwa
sababu ya afya yake, utakuwa umechukuliwa mapema mno.
Kwa hivyo mahakama ya rufaa inaona kuwa mahakama yaliyotangulia kesi
hayakukosa kwa kutozingatia afya ya Bwana Gbagbo katika hali ya sasa."
Bwana Gbagbo anakabili mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu wakati wa
ghasia zilizofuatia uchaguzi miaka miwili iliyopita.
Watu zaidi ya 3000 waliuwawa na malaki walihama makwao, baada ya Bwana Gbagbo
kukataa kwamba alishindwa kwenye uchaguzi. |
0 Comments