Ellinah Wamukoya ameteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa kike wa
kanisa la Kianglikana barani Afrika.
Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa, Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi
huo heshima kwa kina mama.
Ellinah Wamukoya, 61, sasa atahudumu kama askofu mpya wa kanisa hilo katika
ufakme wa Swaziland, moja wapo ya nchi zinazokisiwa kufuata siasaa za
kihafidina.
Kutawazwa kwake kumejiri huku kanisa la Kianglikana, likitarajiwa kujadili
ikiwa kina mama wataruhusiwa kuapishwa kuwa maaskofu wa kanisa hilo.
Askofu wa jimbo la Capte Town, nchini Afrika Kusini, amesema kuwa wamechukua
uamuzi huo ili wawe mfano kwa wengine na pia kuwatakia, viongozi wa kanisa hilo,
faraja na hekima ili kujadilia sauala hilo kwa haraka.
Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa vyo,bo vya habari, askofu huyo wa jimbo la
Cape Town, Revd. Thabo Makgoba, amesema wimbi kwa sasa linavuma na kuwa
wameshuhudia tukio la kihistoria ambao ni sawa na bingu kufunguka.
David Dinkebogile aliongoza sherehe hizo na kukariri kuwa nia yao kuwa
ilikuwa kumuapisha askofu na wale sio mtu mweusi, muafrika na raia wa
Swaziland.
Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa mji mkuu wa Swaziland Manzini. |
0 Comments