Wanajeshi wa Kenya
Maafisa wa matibabu wamesema watu kumi na watano wakiwemo
wanafunzi watatu wamepigwa risasi na kujeruhiwa mjini Garissa Kaskazini
Magharibi mwa Kenya.
Majeruhi hao walipigwa risasi na wanajeshi waliovamia shule hiyo na kuanza
kuwapiga na kuwazuilia watu, baada ya wanajeshi watatu wa Kenya kuuawa na watu
wasiojulikana hapo jana.
Vituo vya kibiashara, shule na ofisi za Serikali zimefungwa huku wanajeshi
hao wakipiga doria katika barabara za mji huo.
Waziri wa Ulinzi wa Kenya Yusuf Haji ameiambia BBC kwamba hakuidhinisha hatua
hiyo ya wanajeshi.
Afisa mkuu wa kimatibabu anayesimamia, hospitali kuu ya mkoa mjini Garisa,
Dkt. Musa Mohamed, ameiambia BBC kuwa watu 45 wamelazwa katika hospital hiyo,
wawili kati yao wakiwa na majeraha ya risasi.
Mapema hii leo, hospitali hiyo pia ilipokea watu wengine kumi na watano
wakiwemo wavulana watatu.
Mmoja wao alikuwa na mareha ya riasi na wanaendelea kupokea matibabu.
Hata hivyo hakuna ripoti yoyote kuhusua maafsa.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limesema kuwa mtu mmoja ameuawa
kwenye machafuko hayo na kuwa shughuli ya kutoa damu ili kuwasaidia wale
waliojeruhiwa inaendelea. |
0 Comments