Muungano wa Afrika AU umeunga mkono mpango wa kuwatuma
wanajeshi wa kutunza amani nchini Mali, kusaidia katika harakati za kupamabana
na wanamgambo wa Kiislamu walioko Kaskazini mwa nchi hiyo.
Kamati kuu wa muungano huo, imeidhinisha uamuzi uliochukuliwa na Muungano wa
Kiuchumi wa nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS wa kutuma wanajeshi 3,000
kusaidia serikali ya Mali, kupambana na waasi hao.
Mpango huo sasa utawasilishwa kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili
kuidhinishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Wapiganaji wa Kiisalmu na wa kabila la Toureq walichukua uthibit wa eneo la
Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya rais wa nchi kuondolewa madarakani kufuatia
mapinduzi yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa wapiganaji hao wa Kiislamu wanataka kutekelezwa
kwa sheria kali za Kiislamu katika maeneo wanayoyathibiti.
Ripoti ya Umoja huo imesema visa vya ndoa vya lazima, vimeongezeka sawia na
wasichana kulazimisha kufanya vitendo vya ukahaba na pia kesi za ubakaji
zimeongezeka.
Muungano huo wa ECOWAS unatarajiwa kudumu kwa muda wa miezi sita, awamu ya
kwanza ikiwa mpango wa kuwapa mafunzo na kujenga kambi Kusini mwa Mali, kabla ya
kuanzisha mikakati ya kijeshi Kaskazini mwa nchi hiyo.
Nchi za Nigeria, Niger na Burkina Faso zimehaidi kutoa wanajeshi hao
watakaotumwa nchini Mali.
Baada ya kuidhinisha mpango hupo, kamishna mkuu wa Usalama na Amani wa
muungano wa Afrika, Ramtane Lamamra, ametoa wito kwa mataifa mengine ya Kiafrika
kutoa wanajeshi zaidi na misaada zaidi ili kufanikisha mpango huu. |
0 Comments