Hivi ndivyo kura zilivyopigwa katika tukio hilo lililojaa shamra shamra za aina yake na kuifanya Palestina kuibuka kidedea na kupandishwa hadhi, kura 138 zilisema ndiyo, kula 9 zilisema hapana na kura 41 hazikufungamana na upande wowote. Tanzania kama ilivyokuwa kwa nchi nyingine nyingi ilipiga kura ya kuunga mkono azimio hilo pamoja na kutoa sababu kwa nini imefikia uamuzi huo. Ingawa azimio hilo linaipandisha hadhi Palestina na kuifungulia milango ya kujiunga na taasisi nyingine za kimataifa, kama ikitaka kufanya hivyo, bado inasafari ndefu ya kufikia hatua ya kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa, kutoka na kwamba ni lazima mchakato huo uanzie Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambako Marekani imeleza bayana kwamba itapiga kura ya veto dhidi ya ombi hilo
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, muda mfupi kabla ya upigaji kura wa Azimio la kuipandisha Hadhi Palestina kuwa kama nchi muangalizi asiye mwanachama wa Umoja wa Mataifa, tukio hilo la kihistoria limefanyika siku ya Alhamisi hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
0 Comments