Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imepuuzilia mbaya makataa iliyotolewa na wapiganaji wa waasi wa kuanzisha mazungumzo ya amani, na kukariri kuwa itaendelea kuilinbda mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi wa M23 wamesemekana kuukaribia mji huo huku maelfu ya raia wakikimbia makwao.
Mapema hii leo, wapiganaji hao walitoa ilaani ya saa ishirini na manne kwa serikali ya nchi hiyo kuanzisha mazungumzo, ya amani la sivyo wataendelea na vita hivyo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa umelaaini hatua hiyo ya waasi wa M23 ya kuendelea na mapigano huku wakielekea mji wa Goma.
Mapigano hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu mwezi Julai Mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Barabaraza mji wa Goma haikuwa na raia kama kawaida na magari ya kijeshi na yale ya umoja wa mataifa ndiyo yaliyokuwa yakizunguka mji huo.
Waasi hao wa M23 wamesema kuwa ikiwa serikali ya nchi hiyo haitakubali kuanzisha mazungumzo hayo, hawatakuwa na budi ila kuendelea na mapigano hayo, hadi watakapoiondoa utawala wa sasa.

Msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende amesema waasi hao wanajumuisha wanajeshi ambao wanaungwa mkono na serikali ya nchi jirani ya Rwanda, ili kuficha vitendo vya kigaidi vinavyoendeleza katika eneo hilo la Mashariki.

Lakini serikali ya Rwanda imepuuzilia mbali madai hayo, ikisema kuwa hayana msingi wowote.