Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa
kwa mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Bi Simone, Gbagbo.
Bi Gbagbo anasakwa kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kivita wakati wa vita
vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka baada ya uchaguzi wa urais nchini humo.
Mumewe tayari amekamatwa na anasubiri kesi yake kuanza katika mahakama hiyo
iliyoko The Haque, kuhusiana na madai hayo ya uhalifu wa kivita.
Takriban watu 3,000 waliuawa kwenye machafuko yaliyotokea baada ya ya Gbagbo
kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa Urais.
Gbagbo na mkewe walikamatwa ndani ya handaki moja Aprili mwaka wa 2011, miezi
mitano, baada ya uchaguzi wa urais.
Wanajeshi wa rais wa sasa wakiungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa
walianzisha msako mkali dhidi yao, baada ya kujificha ndani ya ikulu ya
rais.
anatuhumiwa kuhusika na mauaji, ubakaji, dhuluma na ngona na kuwadhulumu
wapinzani wa serikali miongoni mwa mashtaka mengine mjini Abidjan.
Licha ya kuwa Bi Gbagbo hakuwa akiwania kiti chochote cha kisiasa, ripoti
zinasema kuwa alikuwa na mamlaka makubwa na kuwa alimshawishi mumeo kutokubali
matokeo ya uchaguzi.
Gbagbo, 67, alihamishwa hadi The Haque mwaka uliopita, na kuandikisha
historia ya kuwa rais anayeondoka wa kwanza kufikishwa mbele ya mahakama hiyo ya
ICC.
Rais huyo wa zamani amekanusha madai hayo yote.
Kabla ya kuhamishwa hadi the Haque, Gbagbo na mkewe mwenye umri wa miaka 63,
walifunguliwa mashtaka nchini Ivory Coast kuhusiana na uhalifu wa kiuchumi,
ikiwemo mdai ya kupora mali, wizi wa nguvu na kutumia rasilimali za umma kwa
njia mbaya
Mahakama hiyo ya ICC sasa imetoa wito kwa serikali ya Ivory Coast,
kumusafirisha Bi Gbagbo ili afunguliwa mashtaka huko the Haque. |
0 Comments