Salah Gosh
Watu kadhaa wamekamatwa na serikali ya Sudan, wakiwemo
mkurugenzi mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi, Salah Gosh na maafisa kadhaa wa
jeshi la nchi hiyo kufuatia madai ya kujaribu kupindua serikali ya nchi
hiyo.
Raia kadha wamesema wameona magari kadhaa ya kivita na wanajeshi wakishika
doria katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.
Katika miezi ya hivi karibuni, Utawala wa Khartoum umeshuhudia kuongezeka kwa
maandamano dhidi ya serikali, kupinga kuongezeka kwa bei ya chukula na pia
kushinikiza mabadiliko ya kisiasa.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir amekuwa madarakani tangu mapinduzi ya serikali
mwaka wa 1989.
Waziri wa habari wa Sudan Ahmed Belal Osman, amesema watu 13, wamekamatwa
kuhusiana na njama hiyo ya kupindua serikali. |
0 Comments