Moja kati ya matukio yaliyofurahiwa na watoto ni pale walipoitwa jukwaani kupewa zawadi..zoezi zima la ugawaji wa zawadi liliendeshwa na mzee mzungu(baba Sara) mwenye joho jeupe na miwani.pichani baadhi ya watoto wakipokea zawadi zao.
Baada ya kupewa zawadi kila mtoto alinyanyua mkono wake juu kumuonyesha mzazi wake zawadi aliyopewa.
Kwa upande wa maakuli mambo yalikuwa kama unavyoona..yani ilikuwa ni bandua bandika
                                  Kina mama wakiwa katika utaratibu wa maakuli
Shemeji zetu,dada zetu na mama zetu wakiwa makini kabisa kuhakikisha kila mmoja anapata chakula
             Kuna kipindi cha kubadilishana mawazo na hapo ndipo kama unavyoona
                                           Waaawww.....sector ya maakuli
Bidada Azza katikati akijaribu kumuelewesha mmoja wa wageni wetu aina ya vyakula vya kiafrika..kulia kwa Azza ni Ali Samba mume wa Rahma.
Hawa ni baadhi ya wenyeji wa shughuli
Na kwa upande wa kina baba nao mambo yalikwenda vizuri kabisaa...kila mmoja alikula mpaka akatosheka.Alhamdulillah kwamba shughuli ilikwisha salama.