Mmoja wa polisi waliojeruhiwa, waliletwa Nairobi kwa
matibabu
Takriban polisi 40 wamethibitishwa kuuawa nchini Kenya katika
shambulizi lililofanywa dhidi yao siku ya Jumamosi walipokuwa wanajaribu kuokoa
mifugo waliokuwa wameibwa.
Maafisa hao walivamiwa katika eneo la Baragoi, kaunti ya Samburu, Kaskazini
mwa nchi.
Msemaji wa polisi aliambia BBC kuwa polisi 29 waliuawa pamoja na washambuliji
watatu , lakini viongozi wa kijiji wanahofia kuwa huenda maiti zaidi
wakapatikana. Hii leo miili zaidi ilipatikana na kufikisha idadi ya polisi
waliouawa kuwa 40.
Wenyeji wa eneo hilo wana historia ya kupigana kwa sababu ya uhaba wa malisho
ya mifugo wao
Wiki mbili zilizopita, watu 12 waliuawa katika shambulizi kama hilo kwa
mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya.
Haya yanasemekana kuwa mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea dhidi ya
polisi tangu Kenya kujipatia uhuru wake.
Maiti 11 walipatikana siku ya Jumamosi na wengine 19 kupatikana Jumapili.
Inspekta wawili wakuu wa polisi wangali hawajulikani waliko.
Uvamizi huu ni pigo kubwa kwa idara ya ulinzi nchini. Baadhi ya polisi
waliviziwa na kuuawa na wezi wa mifugo, katika eneo la Lomerok. Manusura tisa
wangali wanapokea matibabu hospitalini.
Mauaji haya yanafikisha idadi ya watu waliouawa katika eneo hilo katika wiki
mbili zilizopita hadi 43.
Aidha mashambulizi haya yanatokea huku shughuli ya kuajiri inspekta mkuu wa
polisi ikiendelea sambamba na polisi kususia kazi kwa sababu ya mzozo wa
mishahara. |
0 Comments