Rais Jakaya Mrisho Kikwete amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho kupisha uchaguzi kufanyika upya. Licha ya kujiuzulu lakini Rais Kikwete anataraji kuchaguliwa tena kwa kishindo kwani ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo ya Uenyekiti.
Kufuatia kujiuzulu huko nafasi ya Uenyekiti imeshikiliwa kwa muda na Rais Mstaafu, Benjamini William Mkapa aliyeungwa mkono na wajumbe wote baada ya jina lake kupendekezwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake.
Mbali na Mwenyekiti pia Sekretarieti yote ya chama hicho imejiuzulu na inasubiri kuchaguliwa tena baada ya uchaguzi kukamilika.
Wadau, mnaonaje hili?

Chanzo cha habari hizi ni
HAPA