Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unafuraha kuwataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa, safari za treni ya abiria ya kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza zitaanza tena kuanzia Desemba 07, 2012 kwa siku za Jumanne na Ijumaa muda wa kuondoka katika Stesheni ya Dar utakuwa saa 8:30 mchana badala ya saa 11:00 jioni.
Hivyo basi , Mwananchi yeyote anayetaka kusafiri kwenda Mwanza anaweza kununua tiketi yake wakati wowote katika Stesheni iliyo karibu naye. Tafadhali atakayesoma taarifa hii amuarifu na mwenzake!

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya


Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu

Dar es Salaam
Novemba 29, 2012