Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-moon ameunga mkono mapendekezo ya Baraza la usalama la umoja wa Mataifa kuidhinisha vikosi vya usalama vya kulinda amani vya AU vipelekwe Mali kukabiliana na wapiganaji wa kiisalamu Kaskazini ya Mali.
Hata hivyo ilikataa kutoa ufadhili wa Umoja wa Matifa katika shughuli hiyo.
Alionya kuwa kuingiliwa kijeshi katika eneo hilo kutasababisha hatari kubwa za kibinadamu na akataka kuwe na mipango ya kutuliza hali hiyo.

Wanadiplomasia wanasema kuwa vikosi hivyo vitatumia nguvu kupita kiasi ilihali vinatakiwa tu kutoa huduma za kusitisha vita kwa njia ya amani.



Hata hivyo bwana Bana hakutoa msaada wa kifedha na ksuema kuwa mataifa ya Afrika yanahitaji maswali kuhusu jeshi hilo litakavyoendesha kazi zake.

Viongozi wa Afrika wamekuwa wakitaka kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kuunda jeshi la pamoja na nchi za Afrika Magharibi litakalosaidia jeshi la Mali kupambana na waasi.

Jeshi la Mali lilipoteza udhibiti wa Kaskazini mwa nchi ambalo linashikiliwa tena.

Kuhusu mapendekezo yake kwa baraza la usalama la umoja huo, bwana Ban alisema ataidhinisha wanachama wa muungano wa Afrika kuunda kikosi cha wanajeshi 3,300 ambao watajulikana kaa AFISMA kuweza kushika doria nchini humo kwa mwaka mmoja.

Alisema wataisaidia jeshi la Mali kurejesha hali ya utulivu kaskazini mwa nchi na kupunguza tisho la makundi ya kigaidi kuvamia eneo hilo