Baada ya kampeni za miezi kadhaa , vituo vya kupiga kura vinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wenye ushindani mkali na ambao ulikuwa na kempeini zenye kugharimu pesa nyingi zaidi kuwahi tumika katika historia za uchaguzi Marekani.
Ushindani katika uchaguzi huu ni mkali sana na mpinzani wa rais Obama wa chama cha Republican Mitt Romney amekuwa akiyazuru mara kwa mara majimbo mawili makuu Ohio na Pennsylvania.

Kura ya mwisho ya kutafuta maoni iliashiria kuwa rais Obama anaongoza katika majimbo mengi ambayo wagombea wote wana nafasi.
Lakini kura hiyo inaashiria pia huenda idadi ya watu watakao jitokeza kupiga kura ikawa kubwa miongoni mwa wafuasi wa Romney
Kura za kwanza zilipigwa katika eneo la Dixville Notch katika jimbo la New Hampshire ambapo wagombea wote walitoka sare.
Rais Obama alitoa wito wake wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa kisiasa uliofanyika katika jimbo la Iowa hapo jana.