Wananchi wakitoroka mapigano
Uingereza imesitisha kwa muda msaada iliyokuwa iipe Rwanda kwa
sababu ya wasiwasi kuhusu kuhusika kwa nchi hiyo katika mzozo uliopo Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Mawaziri walisema kwamba Uingereza sasa haitatoa msaada wa pauni milioni 21.
Rwanda ilipewa msaada wa kiasi cha pauni milioni 16 mnamo mwezi Septemba,
hata baada ya tashwishi kuwepo kuhusu tetesi kwamba ilikuwa inawaunga mkono
wanamgambo wa M23 wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Serikali ya Uingereza ilikuwa imesema kwamba ingetoa kitita kingine cha pauni
milioni 18 kwa ajili ya mahitaji ya kibandamu ya dharura huko Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Makubaliano
Sasa fedha hizo, ambazo zilikuwa zitolewe mwezi ujao, hazitatolewa tena kwa
sababu serikali ya Rais Paul Kagame imekiuka makubaliano.
Nyaraka ya Umoja wa Mataifa iliyofichuliwa inasema kwamba waziri wa ulinzi wa
Rwanda ndiye anayewaamrisha waasi walioko huko.
Mapigano hayo yamepingwa na nchi za kimataifa, huku Marekani na nchi kadhaa
za Ulaya zikizuia msaada uliokuwa umepangwa kwa ajili ya Rwanda.
Waziri Justine Greening wa Uingereza alisema: “Nimeamua kutotoa fedha
zilizokuwa zimekusidiwa kwa ajili ya kuisaidia bajeti ya Rwanda. Ni wajibu wetu
kujaribu kutafuta suluhu za kudumu kwa mzozo wa eneo hili, na kufanya kazi
pamoja na serikali za Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili
kuhakikisha suluhisho la amani linapatikana mashariki mwa Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo." |
0 Comments