Stakabadhi za Serikali zilizotolewa huko Uingereza zinaonyesha
kwa ukamilifu namna wafungwa wengi waliuawa wakati wa uasi wa kundi la Mau Mau
nchini Kenya.
Wakenya kumi na mmoja walipigwa na walinzi hadi kufa katika kambi
walikozuiliwa ya Hola huku wengine wakijeruhiwa mwaka 1959.
Mzee moja manusura wa mauaji hayo kwa sasa ameshtaki serikali ya Uingereza
akidai aliteswa.
Stakabadhi hizo zinaonyesha mkutano uliongozwa na aliyekuwa gavana wa Kenya
na maafisa wakuu wa magereza kumbukumbu zinazoonyesha kuwa maafisa hao walikiuka
haki za binadamu lakini hawakufunguliwa mashtaka. |
0 Comments