Msemaji wa waasi wa M23
Wapigani wa waasi nchini jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
wametishia kuendeleza mapigano hadi mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa, siku chache
tu baada ya kuuteka mji wa Goma.
Msemaji wa kundi hilo la waasi wa M23 rLt Col Vianney Kazarama amewaambia
watu waliokuwa wamekusanyika mjini Goma kuwa wako tayari kukomba taifa hilo.
Awali Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio
linalolaani kutekwa kwa mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na
waasi wa M23.
Azimio hilo pia linamtaka katibu mkuu wa Umoja huo kuripoti kuhusu madai ya
uungwaji mkono wa mataifa ya kigeni kwa makundi ya uasi yaliyoanza harakati zao
nchini Congo miezi minane iliyopita.
Baraza la usalam la Umoja wa mataifa limelaani vikali kitendo cha waasi wa
M23 wa cha kuuteka mji wa Goma.
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa tayari limeidhinisha vikwazo dhidi ya
mkuu wa kundi hilo na limesema limenuia vikwazo hivyo vitawalenga viongozi zaidi
wa waasi .
Wajumbe wa baraza hilo wameelezea hofu kubwa juu ya shutuma kuwa waasi hao
wanaungwa mkono kutoka nje hatua iliyopelekea waasi wa M23 kuwa na uwezo mkubwa
zaidi wa kijeshi
Katibu mkuu wa UN kuchunguza madai
Baraza hilo limemtaka katibu mkuu wa Umoja huo kuchunguza ripoti kuhusiana na
shutuma hizo.
Wataalamu wa Umoja wa mataifa wamesema kuna ushahidi wa kutosha kuwa Rwanda
inawaunga mkono waaasi hao na makundi ya haki za kibinadamu kwa kushindwa kutuma
onyo kwa utawala wa Kigali kama wahusika.
Wakati huo huo maafisa wa Uganda wanasema rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo na rais Paul Kagame wa Rwanda wamekutana nchini Uganda
kujadili Mzozo huo unaoendelea Mashariki mwa Congo .
Mkutano huo wa siku mbili umekuja baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma
Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi hao wanaoaminiwa kuungwa mkono na Rwanda , wanasema wako tayari kusonga
mbele hadi mji mkuu Kinshasa kwa kile walichokitaja kuwa ni kukomboa nchi hiyo
kutoka kwa utawala wa sasa.
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limelaani kukamatwa kwa mji wa Goma |
0 Comments