Bunge nchini Somalia limeidhinisha baraza jipya la mawaziri
kumi waliloteuliwa na waziri mkuu Abdi Farah Shirdon. Wanawake wawili ni
miongoni mwa walioteuliwa.
Serikali kwa mara ya kwanza ina waziri wa kwanza mwanamke atakayeshikilia
wadhifa wa waziri wa mambo ya nje, Fauzia Yusuf Haji Adan na ambaye anatoka
Somaliland.
Kuidhinishwa kwa baraza hilo kumekuja licha ya ripoti kuwa baadhi ya koo
hazikuwakilishwa vyema kwenye baraza hilo liliotajwa wiki moja iliyopita.
"Wabunge walipitisha baraza hilo kwa kura 219 , kati ya wabunge 225,
waliohuduhuria kikao'' alisema spika wa bunge Mohamed Osman Jawari.
Wabunge watatu waliwakataa mawaziri hao huku wengine watatu wakijizuia kupiga
kura.''
Rais mpya pamoja na wabunge wapya walichaguliwa hivi karibuni nchini Somalia
, nchi iliyokuwa haina serikali thabiti kwa zaidi ya miaka 20.
Serikali mpya inakabiliwa na changamoto nyingi wakati ikijaribu kuleta
utulivu na utahbiti katika nchi hiyo ambayo imekumbwa na vita vya muda mrefu
pamoja na tisho la wanamgambo wa Al Shabaab ambao wametishia kuipindua wakisema
inaungwa mkono na nchi za Magharibi. |
0 Comments