Watuhumiwa wakiwa mahakamani kabla ya hukumu kusomwa. kutoka kulia ni Rhoda Robert, Ally Gube na Mohamed Ally.

Mmoja wa ndugu wa Fundikira akibebwa mara baada ya kuzimia na kudondoka sakafuni
Kushoto ni dada wa marehemu Rehema Fundikira, Hadija Mdemu shemeji wa marehemu wakilia mahakamani hapo.

Leo ilikuwa ndiyo siku ya hukumu dhidi ya watuhumiwa watatu wa mauaji ya marehemu Swetu Fundikira aliyeuawa kwa kupigwa miaka miwili iliyopita. Mara baada ya watuhumiwa hao kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa, ndugu na jamaa wa marehemu waliangua kilio na wengine hadi kuzimia kama walivyoshuhudiwa na paparazi wetu aliyeweka kambi mahakamani hapo.