Zaidi ya watu mia mbili sabini wamethibitishwa kufariki katika kimbunga kikali
kinachoendelea kusababisha uharibifu kusini mwa Ufilipino.
Wengine wengi hawajulikani waliko. Nusu ya walioathiriwa walikuwa ni wakaazi
katika maeneo ya milima walioathirika na maporomoka ya udongo baada ya
kuyakimbia makaazi yao ili kwenda kwenye maeneo yalio salama.Katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini humo, Gwendolin Paang,
ameiambia BBC kuwa idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la AP Miili zaidi ya 270 ya watu
waliofariki katika kimbunga hicho ilipokelewa katika maeneo yalioathiriwa na
kimbunga hicho kusini mwa ufilipino.
Kwa mujibu wa maafisa nchini humo huenda miili zaidi ikapatikana katika
maeneo mengine ambayo kwa sasa waokoaji wanaendeleza shughuli za uokozi.
Katika mkoa wa Compostela zaidi ya watu 151 wakiwemo wanajeshi na wenyeji
wameripotiwa kufariki katika mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga hichi cha
bopha .
Zaidi ya watu 80 waliponea kimbunga hicho lakini wengi bado hawajulikani
walipo na wengine zaidi ya elfu 45 wakikosa makao.
Idadi ya vifo hivi vimetokea licha ya rais wa ufilipino Benigno Aquino kutaka
raia wa ufilipino kuhamia maeneo yaliyo salama. Nchi ya ufilipino hukumbwa na
zaidi ya vimbunga 20 kila mwaka |
0 Comments