Nchini Japan chama cha kimuhafidhiin cha Liberal Democratic, LDP, kinaelekea
kushinda kwa viti vingi katika uchaguzi mkuu.Vituo vya kupiga kura baada ya kufungwa, matokeo ya awali yalionesha kuwa LDP
itapata zaidi ya viti 300 katika bunge la viti 480.
Huo ni ushindi mkubwa kwa chama kilichoshindwa vibaya na chama cha mrengo wa
kushoto katika uchaguzi uliopita.
Ni miaka mitatu tu tangu wapigaji kura wa Japani kukitoa madarakani chama cha
LDP kilichotawala kwa miaka mingi, na kukumbatia chama cha Democrat.
Lakini leo wapigaji kura wamebadili maoni - wamekipa kura nyingi sana chama
cha LDP na kukirejesha madarakani.
Waziri Mkuu atakuwa Shinzo Abe, mwanasiasa wa mrengo wa kulia.
Ameahidi kuwa atachukua msimamo mkali dhidi ya Uchina na atapenda kubadilisha
katiba ya Japani, ambayo hairuhusu Japan kuingia katika shughuli za kivita.
Hatua hizo zitaungwa mkono na chama kipya cha Japan Restoration.
Chama hicho kimefanya uzuri na kinaweza kuwa na viti kama 60 kwenye bunge
jipya.
Kama walivotabiri wengi, Japan imebadilisha msimamo na kuelekea kulia. |
0 Comments