Chama tawala cha Afrika kusini, ANC, kimeanza mkutano wake wa taifa leo mjini
Mangaung ambako chama hicho kiliundwa miaka 100 iliyopita.Katika kikao hicho chama kitachagua viongozi wake.
Nje ya ukumbi wa mkutano baadhi ya wajumbe waliimba wakati wamepanga foleni
kuingia ndani.
Rais Jacob Zuma atapambana na naibu wake, Kgalema Motlanthe, kuania
uongozi.
Waandishi wa habari wanasema mkutano huo unafanywa wakati ANC inajitetea
kupata imani ya wafuasi, huku chama kikizungukwa na tuhuma za rushwa kutoka
serikali za mitaa hadi ofisi ya rais. |
0 Comments