Hapo goli la kwanza kwa timu ya Reading lililofungwa kitaalamu na kijana Hal Robson-Kanu wa katikati kulia dk ya 8 ya mchezo.
Dakika chache baadae kijana Anderson wa Manchester United akasawazisha bao kwa mkwaju mkali na mambo yakawa 1-1.
Wayne Rooney akiandika bao la pili kwa njia ya penati baada ya Jonny Evans kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari na hivyo mambo yakawa 2-1 Man inaongoza.
 Adam Le Fondre wa Reading akifunga bao la pili kwa timu ya Reading na kufanya mambo yaende 2-2
Hapo 3-2 Reading wanapata goli la kuongoza baada ya mchezaji wao Sean Morrison kufunga bao kwa njia ya kichwa
Pasi nzuri ya Patrick Evra wa Manchester United inamfanya Wayne Rooney kuandika bao la kusawazishaa kwa Manchester,hivyo mambo yakawa 3-3
Dakika 10 kabla ya mapumziko kijana Robin Van Persie wa Manchester United akiweka mabo sawa kwa timu yake hivyo Manchester wanakwenda mapumziko wakiwa na goli 4-3 dhidi ya Reading.
                                         Kwenye Luninga nako palisomeka hiviiii....

FT West Ham U. 3 - 1 Chelsea
FT Arsenal 0 - 2 Swansea C.
FT Fulham 0 - 3 Tottenham H.
FT Liverpool 1 - 0 Southampton
FT Manchester C. 1 - 1 Everton
FT Queens Park R. 1 - 1 Aston Villa
FT West Bromwich A. 0 - 1 Stoke C.
FT Reading 3 - 4 Manchester U.