Sheria mpya ya Kenya ya kuzuwia madereva kuendesha magari kihatari, inaanza
kutekelezwa Jumamosi.Wakikutikana na makosa madereva watakabili adhabu kali pamoja na kifungo cha
maisha.
Madereva wa mabasi ya abiria, yaani matatu, wamekuwa wakigoma tangu Alhamisi
mjini Nairobi na kwengineko, kulalamika juu ya sheria hiyo.
Wengi wanasema kuwa hawamudu faini kubwa.
Lakini serikali imeazimia kupunguza vifo mabara-barani.
Mwaka uliopita Wakenya zaidi ya 3,000 wamekufa kwenye ajali za
barabarani. |
0 Comments