Wapiganaji wa M23 wa mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wameanza kuondoka katika mji wa Goma ambao waliuteka juma lilopita.Malori yaliyobeba wapiganaji hao yalionekana yakipita kwenye barabara inayotoka Goma kuelekea mji wa Kibumba, ambako wakitarajiwa kukaa baada ya makubaliano yaliyofikiwa mjini Kampala, Uganda.
Hapo awali Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa amri ya vikwazo kuwekewa makamanda wawili wanashutumiwa kuwaajiri watoto kupigana, na kuwauwa wale wanaoasi kundi hilo.
Makamanda hao ni Baudoin Ngaruye na Innocent Kaina.
Rwanda inashutumiwa kuwa inawasaidia wapiganaji hao - shutuma inazokanusha.