Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelezwa hospitali kwa siku ya
pili mjini Pretoria ambako alipelekwa Jumamosi.
Maafisa wamesema kwamba amekuwa akifanyiwa uchunguzi, ingawaje haijajulikana
kwamba ni uchunguzi wa aina gani.
Rais Jacob Zuma, aliyemtembelea Jumapili, alisema kwamba hali yake ilikuwa
nzuri. Bwana Mandela ana miaka 94.
Awali, Mandela alilazwa hospitali mnamo Februari ili kutibiwa matatizo ya
tumbo yaliyokuwa yamemsumbua kwa muda mrefu.
Hajaonekana hadharani tangu Afrika Kusini ilipofungua michezo ya Kombe la
Dunia mwaka wa 2010.
0 Comments