Chama cha upinzani nchini Ghana kimepinga matokeo rasmi ya
uchaguzi mkuu wa urais ambayo yalimpa ushindi rais John Mahama.
Tume ya uchaguzi ilisema kuwa bwana Mahama alishinda kwa asilimia hamsini na
saba ya kura na kuondoa uwezekano wa kufanyika duru ya pili ya uchaguzi huo
dhidi ya mpinzani wake Nana Akufo-Addo aliyepata asilimia 47 ya kura.
Chama cha upinzani New Patriotic Party, kimedai kutokea wizi wa kura na
kusema kitafanya mkutano hapo keshi kuamua hatua watakazochukua.
Ghana imejipa sifa ya kuwa nchi yenye demokrasia thabiti barani Afrika na
moja ya nchi zinazokuwa kwa kasi kubwa barani Afrika.
Kwa upande wake rais Mahama aliwataka watu kuheshimiana kufuatia matangazo ya
kura ambayo yalimpa ushindi.
Hapakuwa na ripoti zozote za ghasia Jumatatu asubuhi baada ya matangazo ya
uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali kutangazwa siku ya Jumapili.
Furaha na nderemo zilijaa punde baada ya matangazo, huku mamia ya watu
wakijitokeza kuonyesha furaha yao kwa ushindi wa rais Mahama. |
0 Comments