Ikulu ya rais wa Afrika Kusini inasema kuwa Nelson Mandela amefanyiwa uperesheni
mjini Pretoria, kutolewa mawe ndani ya kibofu nyongo na anasemekana anaendelea
vizuri.Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 94, alilazwa
hospitali juma moja lilopita kutibiwa mapafu, na ukaguzi ukaonesha mawe hayo
kwenye kibofu.
Katika taarifa iliyotolewa na serikali, imearifiwa kuwa madaktari waliamua
kushughulika na mapafu yake Bwana Mandela kwanza, kabla ya kufanyiwa upersheni
wa Jumamosi.
Wakuu wa Afrika Kusini wamelaumiwa kuwa hawakuwa wakieleza hali ya Bwana
Mandela, ambayo imechochea wasi-wasi zaidi kuhusu afya yake. |
0 Comments