Botswana itapiga marufuku uwindaji halali wa kibiashara wa
wanyamapori ifikapo Januari 2014 kwa sababu ya wasiwasi unaozidi kukua kuhusu
kushuka kwa kasi kwa idadi ya wanyamapori, duru za dola zimesema.
"Kuuwawa kwa wanyamapori kwa ajili ya kujistarehesha tu au kumiliki nyara
haiendi sambamba na nia yetu ya kutunza mazingira nchini," wizara ya mazingira
ilisema.
Marufuku hii inaweza ikazua ubishi kwa sababu ni jamii nyingi ambazo
hutegemea mawindo kama riziki yao.
Takriban thuluthi moja ya ndovu wote duniani wanapatikana nchini Botswana, na
makisio ya hivi majuzi yanakisia kuwa idadi hiyo ni takriban ndovu 130,000.
Watunza mazingira wana wasiwasi kuhusu kumomonyoka kwa kingo za mito
kunakofanywa na wanyama hao mbugani, alisema Letlhogile Lucas, mwandishi habari
wa BBC huko mji mkuu wa Gaborone.
0 Comments