Katika hotuba yake wakati wa kuapishwa kwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Uganda Rais Museveni, alijiepusha kuupinga au kuunga mkono muswada huo.
Rais alisema, ''ikiwa kuna watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, hatutawaua au kuwanyanyasa lakini suala la mapenzi ya jinsia moja halipaswi kuhimizwa katika jamii''
''Hatuwezi kukubali mapenzi ya jinsia moja kupewa msisitizo zaidi katika jamii kana kwamba ni jambo nzuri'' aliongeza rais Museveni.
Mawaziri wamewaonya wabunge kuwa ikiwa watapitisha muswada huo, basi kutakuwa na athari kubwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Uganda na jamii ya kimataifa.
Mataifa ya Magharibi yamelaani muswada huo na wametishia kusitisha misaada kwa Uganda ikiwa itapitishwa na bunge la nchi hiyo.
Spika wa bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amesema muswada huo utapitishwa kama zawadi ya Krismasi kwa mawakili wake.
0 Comments