Njama ya kushambila mkutano wa wajumbe wakuu wa chama tawala
nchini Afrika Kusini, cha African national Congress ANC, imetibuliwa.
Msemaji wa polisi nchini humo amethibitisha tukio hilo, na kusema kuwa
washukiwa wanne wenye asili ya kizungu wenya itikadi za siasa kali
wamekamatwa.
Rais Jacob Zuma, na maafisa wengine wakuu wa serikali na wa chama hicho
wanaohudhuria mkutano huo unaoendelea Mangaung, wamepewa ulinzi mkali.
Viongozi wapya wa chama hicho wanatarajiwa kuchaguliwa na wajumbe hao.
Chama cha ANC, kimekuwa madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa wazungu
walio wachache mwaka wa 1994.
Msemaji wa polisi Phuti Setati, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa
washukiwa wanne ambao walikuwa wakipanga jinsi ya kuuweka bomu katika eneo la
mkutano huo, unaofanyika katika chuo kikuu cha Free State iliyoko katika eneo la
Mangaung.
Zuma kukabiliana na naibu wake
Mwandishi wa BBC Milton Nkosi, ambaye yuko katika eneo hilo anasema, hali ya
ulinzi imeimarisha nje na ndani ya ukumbi wa mkutano huo.
Ameongeza kusema kuwa maafisa wa polisi wanayakagua magari yote na watu
wanaoingia katika ukumbi huo kwa kutumia vifaa maalum na pia mbwa wa kunusa.
Rais Jacob Zuma aliufungua mkutano huo siku ya Jumapili na anawania muhula wa
pili kuwa kiongozi wa chama cha ANC.
Hata hivyo Bwana Zuma, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa naibu wake Kgalema
Motlanthe.
Mmoja wa wafanyabiashara tajiri zaidi nchini Afrika Kusini Cyril Ramaphosa,
amemuunga mkono rais Zuma kwa kuwania kiti cha naibu kiongozi wa chama
hicho.
Bwana Ramaphosa alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliochangia pakubwa
wakati wa mpito kutoka kwa utawala wa kizungu hadi kwa utawa wa Afrika walio
wengi.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, katika eneo hilo la Mangaung, ambako chama
hicho kiliundwa karibu karne moja iliyopita, rais Zum,a alisema kuwa Afrika
Kusini iko tayari kwa awamu ya pili, ambayo atahakikisha kuafikiwa na maendeleo
ya kijamii na kiuchumu yatayaokuwa na manufaa kwa raia wa nchi hiyo.
Matokeo ya uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama hicho yanatarajiwa baadaye
wiki hii. |
0 Comments