my little angle
Pichani ni binti yangu Sharon.
Binti yangu huyu ni mdadisi sana na ana maswali ambayo hupendelea kuniuliza pindi anapokiona kitu ambacho kwake kigeni kwenye fikra zake na hutaka hujifunza.Picha hii nilimpiga kipindi cha kiangazi mwaka 2011,pindi alipotumia muda mwingi kuyaangalia hayo maji yanayomwagika kwa staili yake.alikuwa akiyaangalia huku akivuta hisia ya kitu fulani..sikutaka kumuuliza lolote kwani nilijua kama kawaida yake badala ya kumuuliza ataniuliza kwani ndio utaratibu wake.
 
Haikuwa vile nilivyotarajia...nilipomuita na kumuomba tuendelee na safari yetu hakusita kugeuka na tukaendelea na safari yetu.Nilitarajia swali litakuja mbeleni na hivyo nikawa najipanga kumjibu swali au maswali yake atakayoniuliza kuhusu utazamaji wa maji yale.Mpaka tunafika safari yetu hakukuwa na swali lolote kuhusiana na maji yale.Nikawa najiuliza kwanini leo binti yangu hakuniuliza swali? na sio kawaida yake kukaa kimya pindi akiona kitu ambacho ni kigeni kwenye fikra zake?.Au alikuwa na jibu la kipekee ndani ya fikra zake?au alikuwa hayupo na maji yale kifikra?.hiyo ilikuwa mwaka 2011, binafsi nilijuliza na naendelea kujiuliza kwanini sikuulizwa?
 
Kwa mfano huu ulishajiuliza kuhusiana na mwaka 2012? na kama hukujiuliza unasubiri nani atakuuliza? subiri 2013 pale utakapoulizwa kwanini hukujiuliza na ndipo utakapojiuliza kwanini sikujiuliza kwa kusubiri kuulizwa...?!!
 
Nawatakia jumapili njema.tukutane jumapili ya mwaka  ujao ila sitakuuliza kwanini hukujiuliza kwani hata  mimi sikuulizwa..
                            Maganga One~ Blogger