Ndugu Hija akila kiapo cha uaminifu,upendo na utiifu kwa mkewe mama Leyla mbele ya jaji na mashahidi wengineo walihudhuria sherehe za harusi yao hapo jana jijini Den Haag nchini Uholanzi.
Kwa tabasamu la furaha na upendo mama Leyla akimvisha pete mumewe na kusema kwamba ``wewe ni wangu mpaka kufa``...
 Wachaa weeee..!!!
 Mke na mume wakipata kumbukumbu ya picha
Dj maarufu nchini Holland Dj Key kushoto nae alikuwepo katika kuhakikisha ushahidi wake upo katika harusi mpaka siku ya kiama.
Bwana harusi na bibi harusi pamoja na ndugu,jamaa na marafiki toka sehemu mbalimbali walikuwepo pamoja katika kufanikisha sherehe za harusi zinafanikisha.Ndugu Hija na mkewe wanatoa shukrani za dhati kwa kila mmoja aliyeweza kuja kwenye sherehe zao za harusi hapo jana.Na Maganga One Blogger anasema hongereni sana maharusi na Allah awafanyie wepesi kwa kila jambo insh`Allah.
Bidada Mariam Bim kushoto akiwa na shosti wake ambaye ni bi harusi mama Leyla wakipata picha ya kumbukumbu siku ya jana..
Mariam Bim kushoto,mama Leyla(bi harusi)na mama Samantha wakila pozi moja matata jana kwenye sherehe za miaka 5 ya ndoa ya Hija na mkewe.
Kutoka kushoto ni Jaji aliyefungisha ndoa,msaidizi wa jaji,mama Leyla,Hija na mtoto wao Leyla..Leyla ni matunda ya miaka 5 ya ndoa yao toka walipooana.