Siku ya leo nitazungumzia baadhi ya mambo ambayo jamii inakosea bila kufahamu kwa watoto wetu.
Siku za hivi karibuni kumeongezeka wimbi la malumbano katika familia zetu na hali hii imekuwa kama ni fashion kwa jamii zetu.Moja ya sifa ya mwanaume nijuavyo mimi ni kuwa kiongozi bora katika familia ili kuleta msingi mzuri kwa watoto siku za usoni.

Tofauti na mtazamo wangu nimekuwa nikiona mambo mengi katika familia tofautitofauti hasa katika hii New Generations ambayo ina mambo mengi ambayo sio mazuri kwa jamii.Vijana wengi hata baadhi ya watu wa makamo wamekuwa hawana kauli nzuri kwa wake zao wanapokuwa nyumbani,mke kupigwa na kutukanwa mbele ya watoto imekuwa ndio kama mfumo wa kisasa kwa jamii.

Moja ya makosa makubwa katika familia ni kumvunjia heshima mkeo mbele ya watoto,ninaposema kumvunjia heshima mkeo sio tu kumtukana mbele za watoto,kuna aina nyingi za hukosefu wa heshima kwa wake zetu...Unapoonyesha dharau aina yoyote kwa mkeo mbele ya watoto hiyo ni moja ya hukosefu wa heshima..Unapobwatizana na mkeo mbele ya watoto nao ni ukosefu wa heshima,sasa kuna wengine ambao nawaita wapungufu wa fikra,hekima na busara wanadiriki kuwapiga wake zao mbele ya watoto.

Nakumbuka enzi za nyuma kidogo kwa upande wa wazee wetu mtaani sikuwahi kuwaona wakiwa wanazozana na wake zao hovyo,na kila nilipopata bahati ya kukaa na wazee tulikuwa tukihadithiwa hadithi zao za zamani na jinsi ya kuishi vyema na watoto wetu siku za usoni.

Vijana wengi siku hizi hawana maadili mema katika ndoa,kwa mtazamo wangu wa harakaharaka ni kwamba vijana wengi wanakurupuka katika maamuzi ya kufunga ndoa ili tu kujiridhisha yeye mwenyewe au kumridhisha msichana ambaye anampenda.Utofauti ni mkubwa sana na zamani ambapo wazee wetu walikuwa wakikaa na kutafakari mara mbilimbili kabla ya kuwaingia wazee wao na kutaka ushauri juu ya suala zima la ndoa.

Siku hizi vijana walio wengi wanajichukulia maamuzi wao wenyewe bila kutaka ushauri kutoka kwa wazazi wao au hata waliowatangulia katika masuala ya ndoa.Na matokeo yake huwa wanaona ndoa ni jambo gumu sana tofauti na matarajio yao,au anaweza kuiona ndoa ngumu kulingana na anavyowaona wengine wanavyoishi kwa raha mustarehe.

Siku za hivi karibuni vijana wengi wamebahatika kukamata cent mapema hivyo dharau za  kutaka ushauri kutoka kwa wazee wao inakuwa ni kubwa kwani wanapoona kuwa wazee hawana uwezo basi hutumia nasafi hiyo kama advantage,wanajua kwamba nitakachosema kwa wazee wangu hakitapigwa kwani ni mimi ndio wanaonitegemea katika milo yao ya kila siku.Hilo ni kosa,kumbuka wazee wako ni wazee wako na unapaswa kuwasikiliza kwa hali yoyote.

Narudi kwenye mada yetu,Mwanaume kama mwanaume unayeaminiwa katika familia yako na mkeo jitahidi kadri unavyoweza kuwa na nidhamu nyumbani kwako kwanza.Unapokuwa na nidhamu nyumbani kwako basi hata kazini na kwengineko hali itakuwa ni hivyohivyo na utaonekana bora kwa nidhamu yako.Usije ukajiona mbabe au mjanja unapokwaruzana na mkeo mbele ya watoto.. kwanza ukumbuke hata mtoto/watoto watamdharau mama yao kwa ujinga ulioufanya wewe siku za nyuma kwa kumuonyesha dharau mkeo mbele yao.Hakuna sababu za kujiona mwamba mbele ya mkeo,mwanamke ni kiumbe dhaifu hivyo wanajua kwamba wanaume ni viumbe vya kuheshimiwa na hilo halina mjadala.Sasa basi huna sababu za kujifanya bingwa wa matusi,huna sababu za kumfokea mkeo mbele ya watoto kwani kwa kufanya hivyo unakuwa unaponguza heshima kwa mkeo na kuwafundisha watoto tabia mbaya siku za usoni.

Napenda kuwasisitiza wanaume wenzangu duniani kote kwamba hata kama una tatizo na mama watoto kuna taratibu nzuri za kuambiana na mahala pake,sio mbele za watoto kwani kwa kufanya hivyo tunawaharibu watoto wetu kisaikolojia.na kingine unapunguza mapenzi kwa mkeo kwa kumdhalilisha mbele ya watoto...kumbuka kwa kumfokea mkeo mbele za watoto kuna uwezekano mkubwa wa kuchukiwa na watoto wako.kwani kwa asilimia kubwa watoto wana mapenzi sana kwa mama kuliko baba...kwa leo naomba niishie hapa.na kwa maelezo yangu haya nahisi mtajifunza mengi jinsi ya kuwaheshimu wake zetu na kuwaonyesha mapenzi.

Tukutane jumapili ijayo kwa mada nyingine za kuelimisha kuhusu utaratibu mzima wa maisha yetu.
                                                     Maganga One ~Blogger.

                                                    email~ magangaone@gmail.com